

30 January 2025, 12:53
Serikali imewataka wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Nduta kurejea nchini kwao kwani kwa sasa usalama wa nchi hiyo umekwisha imarika.
Na Lucas Hoha
Wakimbizi wanaohifadhiwa kwenye kambi ya wakimbizi Nduta iliyopo Wilaya ya Kibondo wamekubali kujiandikisha na kurejea nchini mwao mara baada ya Wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania na mashirika ya kimataifa yanayohudumia wakimbizi kuwahakikishia kuwa burundi ni salama.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wakimbizi hao wamesema wamepokea kwa mikono miwili ujumbe wa kuwataka kurudi kwao ili wasaidie kuleta maendeleo ya nchi yao, huku wakitoa wito kwa wakimbizi wenzao kukubali kurudi kwao.
Awali akitoa ujumbe wa kuwataka kurudi nchini Mwao Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wakimbizi kutoka Wizara ya mambo ya ndani nchini Sudi Mwakibasi amesema Kuna kila sababu za wakimbizi kurudi kwao na kuwa serikali ya Burundi imekubali kuwapokea watu wake.
Sauti ya Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wakimbizi Sudi Mwakibasi
Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wanaohudumia wakimbizi akiwemo mratibu wa idara ya wakimbizi Kanda ya Kigoma John Mwita na wawakilishi wa UNHCR wametoa wito wa wakimbizi hao kuwa wanapoendelea kukaa kambini hapo wanapoteza vitu mhimu katika maisha yao ikiwemo kushindwa kujikwamua kiuchumi
Sauti za viongozi