Kampuni ya itel yatoa vitu vya thamani ya milioni 100 kwa wakimbizi Kasulu
24 January 2025, 17:38
Wadau mbambaili wa maendeleo nchini wameaswa kuendelea kujitokeza kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wakimbizi wanaoishi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu.
Na Emmanuel kamangu
Kampuni ya simu ya itel nchini Tanzania imetoa vitu vyenye thamani ya zaidi million 100 kwa wakimbizi wa kambi ya nyarugusu wilayani kasulu.
Akikabidhi vitu hivyo kwa wakimbizi wa kambi ya nyarugusu wilayalani Kasulu, Meneja masoko wa kampuni ya simu ya itel nchini Tanzania Bi, Sofia Msafiri amevitaja vitu hivyo kuwa ni taulo za wanawake pc 5000, Net za mbu pc 5000, nguo za ndani za wanawake na wanaume 5000 pamoja na kanga pc 5000 na ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo wa kuendelea kukaa karibu na jamii zote zenye kukabiliwa na changamoto mbali mbali.
Kwa upande wake, Mkuu wa kambi ya wakimbizi nyarugusu Bw. Siasa Manjenje kwa niaba ya serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapongeza kampuni ya simu ya itel kwa msaada huo ambao kwa kiasi kikubwa utatatua changamoto nyingi zinazo wakabili wakimbizi katika kambi hiyo.
Matumaini mbogeka na Manailakiza Jafeti ni wakazi wa kambi ya nyarugusu ambao kwa niaba ya wakimbizi wote wameshukuru kampuni ya simu ya itel kwa msaada huo huku wakiomba kampuni zingine kuendelea kujitoa kuwasaidia.