Wananchi wajitokeze kuchangia damu Kasulu
22 January 2025, 12:15
Changia damu okoa maisha ni kaulimbiu ambayo imekuwa ikitumika ili kuhamasisha uchangiaji damu kwa lengo la kuokoa maisha.
Na Michael Mpunije
Waumini wa dini ya Kiislamu kutoka Jumuiya ya Jai wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamefanya matendo ya huruma kwa kuchangia damu pamoja na kutoa msaada wa chakula kwa wagonjwa katika hospitali ya halmashauri ya mji Kasulu Mlimani.
Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Jai wilaya ya Kasulu Ostadhi Abdurahman Nyamgenda amesema lengo la kutoa msaada wa chakula na kuchangia damu ni katika kuokoa maisha ya wagonjwa waofika katika hospitali hiyo.
Sauti ya Mwnyekiti Jai
Kwa upande wake katibu wa Bakwata halmashauri ya mji Kasulu Abeid Buteta amesema wameshirikiana na waumini wengine wa dini ya Kiislamu kutoka Manispaa ya kigoma Ujiji pamoja na wilaya Kasulu katika kuwasaidia baadhi ya wagonjwa wanaofika hospitali na kukosa msaada wa chakula na huduma zingine hali inayosababisha baadhi yao kupitia changamoto mbalimbali.
Sauti ya katibu BAKWATA
Kwa upande wao baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu Aisha Kahuza na Haji Juma Ulimwengu wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa wanaotoka mbali na kulazwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya pamoja na jamii kuwathamini wagonjwa kwa kuwatembelea mara kwamara kutoa Msaada.
Sauti za waumini
Kaimu mganga mkuu Halmashauri ya mji Kasulu Dkt Augustino Karoli amesema jumla Unit 60 za damu zimepatikana huku akiwaomba wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuoa maisha ya wahitaji pamoja na kuendelea kuwasadia wagonjwa mbalimbali wanaofika hospitali.
Sauti ya Kaimu mganga mkuu Halmashauri ya mji Kasulu