Joy FM

Madereva pikipiki waonywa kubeba wahamiaji haramu

15 January 2025, 17:02

Madereva bodaboda wakiwa wamepaki vyombo vya buhigwe, Picha na Mtandao

Serikali ya Tanzania inaendelea kudhibiti wahamiaji haramu kuingia nchini kinyume cha sheria lengo ikiwa ni kukabilia na vitendo vya uhalifu.

Na James Jovin

Madereva boda boda wilayani buhigwe mkoani kigoma wameonywa kuacha tabia ya kubeba wahamiaji haramu na kuwaingiza nchini lakini pia kutojihusisha na biashara za magendo hali inayotishia usalama wa raia hasa mipakani

Wakizungumza na Radio Joy Fm, baadhi ya wananchi wakazi wa wilaya ya buhigwe waliohudhulia mafunzo ya usalama barabarani katika chuo cha veta buhigwe wamekili kukithili kwa tabia hiyo hasa maeneo ya mipakani.

Sauti ya baadhi ya wananchi wakazi wa wilaya ya buhigwe

Aidha mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya buhigwe Noel Moshi pamoja na kaimu mkuu wa wilaya ya buhigwe bi. emma emmanuel wakizungumza wakati wa kuhimitimsha mafunzo ya usalama barabarani chuo cha veta buhigwe wamewataka boda boda kuacha tabia hizo.

Sauti ya mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya buhigwe noel moshi

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha veta buhigwe Bw. Ally Bushiri amesema chuo hicho kimeweka mkakati wa kuhamasisha boda boda wote ili waweze kupata mafunzo ya usalama barabarani lakini pia kufundishwa sheria za nchi ili kudhibiti changamoto hiyo.

Sauti ya Mkuu wa chuo cha veta buhigwe Bw. Ally Bushiri