Joy FM

Bodaboda walia na kamatakamata ya polisi Kigoma

9 January 2025, 16:38

Ni baadhi ya madereva bodaboda mjini wakiwa katika maandamano, Picha na Hamis Ntelekwa

Baadhi ya madereva Bodaboda katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma wamefanya maandamano kupinga kamatakamata ya vyombo  vya  moto inayoendelea Mjini Kigoma na kuomba Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

Wakizungumza na Radio Joy Fm, Baadhi ya madereva hao wamesema wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara kupitia operesheni zinazofanywa na Jeshi la Polisi barabarani na kuwa wanapokamatwa wanatozwa faini bila kupewa lisiti

Wamesema kuna kila sababu za viongozi wa serikali kuingilia kati suala hilo ili waendelea kufanya kazi kwenye mazingira rafiki kwani wanategemea kazi ya bodaboda kupata mahitaji ya familia na kusomesha watoto.

Sauti ya baadhi ya madereva bodaboda mjini Kigoma wakilalamikia vitendo vya kukamatwa

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Filemon Makungu amekiri kuwepo kwa kamatakamata ya Madereva bodaboda na kuwa zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha madereva hao wanafuata kanuni na sharia za usalama barabara.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Filemon Makungu