Ajali ya moto yaua wawili na mmoja kujeruhiwa
2 January 2025, 12:11
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kigoma limewataka wananchi kuacha kuhifadhi vilipuzi ndani za makazi ili kuepuka ajali za moto zinazoweza kujitokeza.
Na Orida Sayon – Kigoma
Watoto wawili wa familia moja wamefariki na baba kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea katika kijiji cha Pamila halmashauri ya wilaya ya Kigoma.
Kaimu Kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kigoma Michael Maganga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo chanzo cha ajali ni mlipuko wa mafuta aina ya petroli yaliyokuwa yamehifadhiwa ndani ya nyumba na kusababisha vifo hivyo vilivyosababishwa wakiwa wamelala.
Aidha Maganga amewataka wananchi kuendelea kujikinga na ajali zinazoepukika kwa kuacha kutunza vilipuzi ndani ya nyumba na kutoa taarifa kwa wakati pale ajali zinapotokea.
Mtoa huduma za afya kijijini hapo Sospeter Gunzali alimpokea mama wa familia iliyopata ajari hiyo baada ya kupata mshituko na hapa anaeleza.
Mwenyekiti wa kijiji cha pamila Jumanne Kavungwe amekiri kutokea kwa ajali hiyo huku baadhi ya wananchi walioshuhudia wakaeleza namna ajali hiyo ilivyotokea na hisia zao juu ya tukio hilo.