Joy FM

Viwavijeshi vyashambulia mazao ya wakulima Kigoma

18 December 2024, 09:25

Muonekano wa mahindi shambani baada ya kushambuliwa na wadudu, Picha na Emmanuel Michael Seny

Wakulima katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuzingatia matumizi ya mbegu bora za kilimo zinazohimili magonjwa na kutumia viwatilifu ili kusaidia kukabiliana na wadudu wanaoshambulia mashamba.

Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma

Mashamba ya mahindi katika Halmashauri za Wilaya ya Kigoma na Uvinza Mkoani Kigoma yamevamiwa na wadudu maarufu viwavijeshi wasumbufu ambao wanashambulia majani na mimea na kuathiri ukuwaji wa mahindi, ambapo wakulima wameomba hatua za haraka ikiwemo upatikanaji wa dawa za kuua wadudu hao ili kuepusha athari za kukosa mazao ya mahindi.

Wadudu hao maarufu viwavijeshi wasumbufu, hushambulia mmea kwa ndani na majani na kuhafifisha ukuwaji hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao.

Muonekano wa mahindi shambani baada ya kushambuliwa na wadudu, Picha na Emmanuel Michael Seny

Wakulima wanalazimika kuomba hatua za haraka, kubaini dawa za kuua wadudu hao ambao wanatajwa kushambulia mashamba ya mahindi.

Sauti ya wakulima wa zao la mahindi kutoka wilaya za Uvinza na Kigoma

Katika kikao cha watafiti wa mazao ya kilimo, kutoka taasisi za utafiti wa mbegu za kilimo Tanzania, kituo cha Tumbi Tabora, TARI Kihinga Kigoma pamoja na Makao makuu Dodoma wamewataka wakulima kutumia mbegu bora zinazokinzana na magonjwa na kuepusha mazao kushambuliwa na wadudu, sambamba na kubainisha hatua zinazochukuliwa dhidi ya wadudu wanaoshambulia mazao.

Sauti ya watafiti wa mazao ya kilimo, kutoka taasisi za utafiti wa mbegu za kilimo Tanzania, kituo cha Tumbi Tabora, TARI Kihinga Kigoma pamoja na Makao makuu Dodoma
Muonekano wa shamba la mahindi ya wakulima halmashauri ya wilaya Kigoma, Picha na Emmanuel Senny