Joy FM

Waumini wa dini ya kikristo watakiwa kiliombea Taifa

11 December 2024, 11:32

Pichani ni Askofu kanisa la Anglikana dayosisi ya western Tangnyika Mhashamu Emmanuel Bwatta, picha na Hagayi Ruyagila.

Kuendelea kupiga vita vitendo vya ukatili Viongozi wa dini wameendelea kuwasisitiza waumini wa madhehebu mbalimbali kuliombea Taifa.

Waumini wa dini ya kikristo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuliombea taifa la Tanzania kuendelea kuwa na amani ili kuepuka vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji na utekaji ambavyo vinaripotiwa katika baadhi ya maeneo hapa nchi.

Hayo yameelezwa na Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Anglikana Kabanga lililopo Mjini Kasulu Mkoani Kigoma.

Amesema suala la uchaguzi tayari limemalizika hivyo wananchi wanatakiwa kuendeea kuliombea taifa ili kuepuka vitendo hivyo ambavyo havipendezi katika jamii.

Sauti ya Askofu Bwatta

Kwa upande wake mkurugenzi wa kanda ya kasulu mjini wa kanisa la anglikana Murusi Mchungaji Canon Laurent Magogwa amesema jamii inapaswa kuishi maisha mema ya kuthaminiana kwa kuonyesha upendo kwa mwingine ili yashinda matendo hayo yasiyofaa.

Pichani ni Mchungaji Canon Laurent Magogwa, Picha na Hagayi Ruyagila

Sauti ya Mchungaji Canon Laurent Magogwa

Nao baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo wamesema ni vivyema serikali ikafanya uchunguzi kuhusu suala hilo ili atakae bainika aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Sauti za Waumini