Joy FM

Umasikini watajwa kuwa chanzo cha ukatili Kigoma

10 December 2024, 16:36

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta, Picha na Hagai Ruyagila

Wakati elimu mbalimbali ikiendelea kutolewa juu ya vitendo vya ukatili, jamii imetakiwa kuwa pamoja na kutoa taarifa za vitendo hivyo.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Inaelezwa kuwa kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, watoto pamoja na wanaume kunatokana na sababu za kiuchumi kutokana na kipato kidogo katika familia pamoja na mifumo ya maisha jambo ambalo serikali na taasisi za kupinga ukatili zinapaswa kutoa elimu ili kuleta ustawi bora katika jamii.

Hayo yameelezwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta wakati akizungumza na Radio Joy FM ambapo amesema ukatili wa kijinsia umeendelea kuongezeka  kutokana na mifumo mibovu isiyofaa ndani ya jamii.

Askofu Emmanuel Bwatta

Aidha Askofu Bwatta amesema ili kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia serikali inapaswa kuungana na taasisi binafsi ili kuendelea kupeleka elimu kwa jamii kuhusu madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia.

Askofu Emmanuel Bwatta

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanda ya Kasulu Mjini wa kanisa hilo Murusi Mchungaji Canon Laurent Magogwa amesema ili jamii kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili inapaswa kuishi maisha ya kumpenda na kumcha Mungu.

Mchungaji Canon Laurent Magogwa

Nao baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamesema ukatili wa kijinsia unasababishwa na baadhi ya wananchi kukosa elimu ya masuala ya ukatii hali inayopelekea kushindwa kutoa ushirikiano kwa serikali.

Wananchi