Watoto wajengewe msingi mzuri wa masomo
5 December 2024, 13:30
Ili watoto waweze kufikia ndoto zao wazazi wanapaswa kuwekeza katika msingi iliyo imara katika masomo.
Na Prisca Kizeba – Kigoma
Askofu Mkuu wa Makanisa ya New Hope ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule ya Kembrigi Josphat Njige amewataka wazazi kuwajengea watoto wao msingi mzuri wa kimasomo ili kuwa na mwelekeo mzuri wa kielimu.
Njige ameyasema hayo wakati wa mahafali ya watoto wa chekechea katika shule ya kembrigi iliyopo manispaa ya kigoma ujiji na kuwa ili mtoto aweze kuwa na mwelekeo mzuri wa kimasomo ni lazima ajengewe msingi mzuri wa awali.
Sauti ya Askofu na Mkurugenzi wa shule ya awali Cambridgeshire
Naye mratibu wa kituo hicho cha shule Magreth Mpataleo Mushi ambaye pia ni Mwalimu amesema kuwa zipo changamo ambazo wanakuta nazo watoto kwa mfano hali ya upweke kutokana na migogoro ya kifamili.
Sauti ya mratibu wa kituo Magreth Mpateleo
Nao badhi ya wazazi akiwemo Athoni Jacobo na Witnes Mussa wariohundhuria mahafali hayo wamewashukuru walimu kwakuwajengea msingi mzuri watoto wao.