Wazazi, walezi pingeni vitendo vya ukatili kwa watoto
5 December 2024, 12:19
Wadau mbalimbali mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kushirikiana na Serikali kupinga vitendo vya ukatili katika maeneo yote
Na Orida Sayon-Kigoma
Wazazi na walezi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kukaa na watoto wao na kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia ili kuwasaidia kutofanyiwa vitendo vya ukatili.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Joy In the Harvest na Radio Joy Mwenge Muyombi katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne shule ya sekondari Kigoma Ujiji yaliyofanyika katika ukumbi wa kanisa la Anglikana ambapo amesema wananchi wote wanapaswa kupiga vita vitendo vya ukatili kwani vimekuwa na madhara makubwa kwenye jamii.
Sauti ya Mkurugenzi wa Joy in the Harvest Mwenge Muyombi
Naye Karume Amani Rashidi kutoka Shirika la Kijana Mzalendo na jamii endelevu Tanzania (KIMJAE) amewaasa wahitimu hao kuwa wazalendo kwa kuzidisha maadili mema kwenye jamii.
Kwa upande wake, mkuu wa shule ya sekondari Kigoma Ujiji Bw. Malaki Amoni ameeleza namna wanavyodhibiti vitendo vya ukatili katika mazingira ya shule na kuendelea kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwapa ushirikiano wa kimalezi walimu.
Baadhi ya wazazi wa wahitimu hao wakazungumza namna wanavyowalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili hasa wawapo katika mazingira ya nyumbani.
Hata hivyo wahitimu hao wameeleza namna elimu waliyopata itakavyowasaidia.