Joy FM

Mwalimu kutumia siku nane kusafiri kwa baiskeli Kigoma hadi Dodoma

2 December 2024, 15:42

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ijunga Halmshauri ya Kasulu mji Wenseslaus Lugaya ameamua kutumia usafiri wa baiskeli kutoka Kigoma hadi jijini Dodoma lengo likiwa ni kutangaza miradi ambayo inatekelezwa ndani ya serikali ya awamu ya sita sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira na anatarajia kupokelewa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Disemba 09, 2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru.

Taarifa zaidi na Josephine Kiravu

Akizungumza wakati wa kumuaga mwalimu huyo,  Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewataka vijana kutoona haya kutungaza yale mazuri ambayo yamefanywa na Serikali ya awamu ya sita.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye

Kwa upande wake, Mwalimu Wenseslaus Lugaya maarufu kwa jina la Gadafi ameeleza adhima ya safari yake huku akieleza baadhi ya miradi ambayo imemvutia na kumfanya kufunga safari hadi Dodoma kumpongeza Rais.

Mwalimu Wenseslaus Lugaya

Mwalimu Wenseslaus Lugaya maarufu Gadafi ameanza safari yake rasmi hapo jana kuelekea Jijini Dodoma ambapo anatarajia kutumia muda wa siku nane huku akiamini atawafikia wananchi kwa kiasi kikubwa na kuwapatia elimu kuhusu mambo kadhaa ikiwemo kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kujikita kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.