Viongozi serikali za mitaa watakiwa kulinda amani na usalama
2 December 2024, 12:44
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wametakiwa kuhakikisha wanalinda amani na usala katika maeneo yao.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanal Isaac Mwakisu amewataka viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji waliochaguliwa kuhakikisha wanalinda amani na usalama katika ameneo yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na nchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wenyeviti wa vijiji, vitongoji pamoja na wajumbe waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu wakati wa zoezi la kuwaapisha viongozi hao.
Kanal Mwakisu amesema kila kiongozi anapaswa kusimamia ulinzi, usalma pamoja na miradi yote inayokuja katika maeneo yao bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dr. Semistatus Mashimba amewasisitiza kuondoa tofauti zao za vyama vya siasa badala yake kuwa kitu kimoja ili kumsaidia kazi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi walizo chaguliwa.
Hakimu wa mahakama ya mwanzo wilaya ya Kasulu Rajabu Mtuli amesema nafasi hiyo waliyochaguiwa viongozi hao ni yamuhimu sana katika jamii maana inasaidia kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo migogoro ya ardhi.
Nao baadhi ya viongozi waliochaguliwa kutoka halmashauri ya wilaya ya Kasulu wamesema watahakikisha wanasimamia ulinzi na usalama pamoja na miradi inayopelekwa na serikali katika maeneo yao.
Ni baadhi ya viongozi waliochaguliwa kutoka halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila