Joy FM

Serikali yatenga fedha utatuzi wa changamoto ya umeme Kigoma

21 November 2024, 09:36

Wanachama wa chama cha mapinduzi wakiwa katika mkutuno wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali imesema tayari imekwisha tenga fedha za kuhakikisha inatatua changamoto zaukosefu wa umeme kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma ili kuhakikisha umeme wa uhakika unakuwepo kupitia gridi ya Taifa.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa amesema serikali tayari imetenga fedha ili kutatua changamoto ya huduma ya umeme na migogoro ya ardhi iliyopo katika mkoa wa Kigoma

Katika uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kigoma ambapo Waziri Mkuu Majaliwa aliyewakilishwa na mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM, Mh Christopher Gachuma amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo katika uwanja wa Kiganamo uliopo Mjini Kasulu mkoani Kigoma.

Sauti ya mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM, Mh Christopher Gachuma

Aidha Gachuma amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi kuvunja makundi yaliyopo ndani ya chama hicho ili kumuamini mgombea mmoja aliyeteuliwa na chama hali itakayosaidia kufanya vizuri katika uchaguzi.

Mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM, Mh Christopher Gachuma, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Jamali Tamimu amesema ili kufanya vizuri katika uchaguzi wa uongozi wa serikali za mitaa wanatakiwa kuwa kitu kimoja maana serikali imefanya mambo mengi ya maendeleo katika mkoa wa Kigoma.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Jamali Tamimu

Nao baadhi ya wabunge wa mkoa wa Kigoma wakiwakilishwa na mbunge wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako wamesema serikali imefanya mambo mengi ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo miundombinu ya barabara, sekta ya afya pamoja na sekta ya elimu.

Sauti ya wabunge wa mkoa wa Kigoma wakiwakilishwa na mbunge wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako
Mbunge wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako, Picha na Hagai Ruyagila

Uchaguzi wa serikali za mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu huku Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu wa 2024 umebebwa na kauli mbiu isemayo serikali za mitaa sauti ya wananchi jitokezeni kushiriki uchaguzi kwa maendeleo endelevu.