Joy FM

Vuta nikuvute urejeshaji maeneo ya serikali Kigoma

18 November 2024, 08:44

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Kisena Mabuba amewahakikishia  madiwani wa Manispaa hiyo kuwa anasimamia kwa nguvu ili kuhakikisha maeneo ya wazi yanayomilikiwa na Manispaa yanapatiwa hati miliki ili kuepuka maeneo hayo kuvamiwa na watu wasio waaminifu.

Na, Lucas Hoha

Bw. Mabuba ameyasema hayo  kwenye baraza la madiwani mara baada ya madiwani kutoa hoja mbalimbali zilizolenga kufahamu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uvamizi wa maeneo ya wazi yanayomilikiwa  na Manispaa ambapo amesema maeneo ya wazi na maeneo yote yenye taasisi za serikali atahakikisha yanapatiwa hati miliki.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Kisena Mabuba

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Baraka Lupoli amesema changamoto hiyo ya watu kuvamia maeneo ya wazi ni yamuda mrefu na ilikuwa imeshindwa kupatiwa ufumbuzi, huku akiwaomba madiwani kuendelea kumpa ushirikiano mkurugenzi ili kuyatambua maeneo ya wazi.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Baraka Lupoli

Awali baadhi ya Madiwani walihoji kutaka kufahamu mikakati ya Ofisi ya Mkurugenzi katika kuhakikisha inayatambua maeneo ya wazi yanayovamiwa nakuyapatia hatimiliki kama wanavyosema.

Madiwani