DC Kasulu awafunda madiwani kuelekea uchaguzi
15 November 2024, 15:00
Zikiwa zimebaikia siku 12 kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mkuu wa wilaya ya kasulu kanal Isack mwakisu amewataka madiwani wilayani humo kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuwahimiza wananchi wajitokeze kuwachagua viongozi wao.
Kanal mwakisu amesema hayo katika mkutano wa baraza la madiwani kipindi cha robo ya kwanza ya july hadi septeber 24,25 ambapo amewaomba madiwani kuwashawishi wananchi bila kutumia nguvu ili kuhakikisha wanajitokeza kikamilifu siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha kanal mwakisu amewataka madiwani kuhakikisha wanaihubiri amani wakati huu wa uchaguzi ili kuepuka munyukano unaoweza kuhatarisha amani ya Tanzania.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kasulu Bw,Elia kagoma amewaomba wagombea kutumia lugha nzuri na zaidi kueleza sera zao kuliko kutumia kauli zinazoweza kupelekea vurugu.
Hata hivyo madiwani kwa ujumla wameaswa kuhakikisha wanazingatia r 4 za rais daktari samia suruhu hasani kwa kuhubiri ustahimilivu,usuruhishi, mabadiliko na kujenga upya umoja wetu.