Joy FM

Madaktari bingwa waweka kambi hospitali ya rufaa maweni Kigoma

28 October 2024, 15:32

Baadhi ya madaktari bingwa walioweka kambi haspitali ya rufaa maweni Kigoma wakiwa na Mkuu wa Mkoa Kigoma, Picha na Lucas Hoha

Madaktari bingwa na mabingwa bobezi  31 wameanza Kambi ya  matibabu ya Siku Tano ikiwa ni katika kuadhimisha miaka Hamsini (50) tangu kuanzishwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni. 

Na Lucas Hoha – Kigoma

Wananchi Mkoani Kigoma wamepongeza jitihada za serikali za kuendeleza kusogeza huduma za matibabu  karibu na Maeneo yao ikiwemo matibabu ya kibingwa ambayo yamekuwa yakitolewa kwa wananchi Mkoa hapa.

Wananchi hao wamesema hayo mara baada ya uzinduzi wa kambi ya madaktari bingwa na madaktari bingwa bobezi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni na kuwa ujio wa mabingwa hao utasaidia kuwapunguzia gharama kwani awali walikuwa wanashindwa kufuata huduma hizo kutokana na kipato kidogo.

Wananchi Mkoani Kigoma walifika kupata huduma za afya ambazo zinatolewa na kambi ya madaktari bingwa, Picha na Lucas Hoha  
Sauti za wananchi Mkoani Kigoma

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amesema serikali imedhamilia kwa dhati kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya zenye uhakika, huku akiwaomba wananchi kujitokeza kupata matibabu hayo ili wawe na Afya bora.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye, Picha na Lucas Hoha
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Nao baadhi ya viongozi wa kada ya Afya walioshiriki kwenye uzinduzi huo akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Damas Kayera wamesema kupitia kambi hizo zaidi ya wananchi elfu 8000 watapatiwa matibabu ya kibingwa.

Sauti ya baadhi ya viongozi wa kada ya Afya walioshiriki kwenye uzinduzi huo

Katika kambi hiyo ya siku tano jumla ya madaktari bingwa 31 watatoa huduma za kibingwa na miongoni mwa matibabu yatakayotolewa ni magonjwa ya wanawake, Saratani, magomjwa ya moyo, upasuaji na magonjwa ya kinywa na meno.