Wananchi Buhigwe walalamikia mradi mpya wa maji
25 October 2024, 09:49
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kinazi wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wameiomba serikali kukarabati mradi wa maji wa zamani ambao ulikuwa ukitoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo baada ya mradi wa maji wa sasa kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati.
Na, Michael Mpunije
Wananchi wa kata ya Kinazi baada kuona mradi wa wa maji wa sasa hautoi huduma hiyo kwa wakati wameomba kuendeleza mradi wao wa zamani ili kuondoa usumbufu wa kufuata maji umbali mrefu.
Wamesema wapo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha huduma ya maji inapatikana ndani ya kata hiyo yenye vijiji viwili vya kinazi na Kimara kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Diwani wa kata ya Kinazi Bw.Yusuph Degede akizungumza na wananchi wa kata hiyo amesema anaitambua changamoto ya maji kwenye kata yake na kwamba upo mchakato wa Serikali wa kurejesha mradi huo wa zamani licha yakuwa chanzo chake kimeshaharibika.
Aidha amesisitiza wananchi kuhudhuria mikutano ya hadhara inapoitishwa kwa ajili ya kujadili masuala ya maendeleo ya kata ili kutafta namna bora ya kufikia malengo yakutatua changamoto zilizopo katika kata hiyo.