Joy FM

Polisi Kigoma yawataka wananchi kusalimisha silaha

16 October 2024, 12:55

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Filemon Makungu, Picha na Josephine Kiravu

Jeshi la polisi Mkoani Kigoma limewataka wananchi ambao hawajasalimisha silaha zao kufanya hivyo kwani muda wa kusalimisha ukiisha msako mkali utaanza ili kuwabaini wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Na Josephine Kiravu – Kigoma

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kusalimisha kwa hiari silaha ambazo wanamiliki kinyume na sheria kabla ya muda wa msamaha uliotolewa kutamatika.

Hayo yameelezwa na kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Filemon Makungu wakati akieleza mafanikio ya misako na operesheni mbalimbali zilizofanyika kuanzia Septemba 17 mwaka huu hadi Oktoba 14 mwaka huu.

Amesema tangu kuanza kwa zoezi la usalimishaji wa silaha kwa hiari ni mwananchi mmoja pekee ambae amesalimisha silaha aina ya AK 47 aliyokuwa akimiliki kinyume na sheria.

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Filemon Makungu

Katika hatua nyingine Kamanda Makungu amesema wamefanikiwa kukamata kilo 500 za bhangi sambamba na wahamiaji haramu 104 ambao waliingia na kuishi nchini kinyume na sheria.

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Filemon Makungu

Hata hivyo kufuatia wananchi kuendelea kujichukulia sheria mkononi jeshi la polisi limetoa elimu kwa wananchi na kuwataka kuacha mara moja kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Filemon Makungu

Jeshi la polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu matukioa ya uhalifu na wahalifu pasipo kuchukua sheria mkononi ili kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, SACP Filemon Makungu, Picha na Josephine Kiravu