Joy FM

Meli ya MT Sangara kukabidhiwa serikalini Kigoma

19 September 2024, 14:29

Muonekano wa meli ya MT Sangara inayofanyiwa ukarabati ndani ya ziwa Tanganyika, Picha na Mtandao

Meli ya Mafuta ya MT Sangara iliyokuwa katika ukarabati mkubwa imefanyiwa ukaguzi na majaribio ya mwisho ya mitambo yake ikiwa katika asilimia 96% kabla ya kukamilika na kukabidhiwa serikalini ili kuanza kazi zake katika Ziwa Tanganyika.

Na, Emmanuel Matinde

Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 380 sawa na lita laki nne na elfu kumi za mafuta ilisimama kufanya kazi tangu Octoba mwaka 2020 kutokana na uchakavu wa mitambo ya Injini ambapo kutokana na umuhimu wake serikali iliamua kutoa fedha Shilingi Bilioni 8.4 ili kuifanyia ukarabati.

Mhandisi wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania MSCL ambaye ni Msimamizi wa Mradi wa Meli ya MT Sangara Mhandisi wa David Jenga, ameeleza kitaalam matengenezo yaliyofanyika katika Meli hiyo.

Meli ya MT Sangara inatoa huduma ya kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Kigoma kwenda Bandari za Kalemie na Uvira katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na nchi ya Burundi.

Miongoni mwa matokeo ya ukarabati wa meli hiyo yanayotarajiwa ni kupungua kwa gharama za usafirishaji hivyo kuiwezesha MSCL kukabiliana vyema na ushindani wa masoko dhidi ya kampuni nyingine kama anavyoelezwa Kaimu Meneja MSCL Tawi la Kigoma Allen Butembero.

Kaimu Meneja MSCL Tawi la Kigoma Allen Butembero

..