Vijana kuongeza mchango wa kilimo kwenye Taifa
17 September 2024, 14:53
Serikali wilayani kibondo imesema vijana hawana budi kuchangamkia fursa za kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuacha kupoteza muda kusubiri ajira.
Na James Jovin – Kibondo
Vijana wilayani Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa kuwekeza katika sekta ya kilimo ili kujikwamua kimaisha kwa kuwa kilimo ni sekta iliyoajili Zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wote kote nchini huku serikali ikiwa tayari imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa vijana
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya kilimo,mifugo na uvuvi wilayani Kibondo Dr. Gabriel Chitupila wakati wa kongamano la vijana kuelekea mwenge wa uhuru 2024 lililofanyika mjini kibondo.
Kwa upande wake afisa tarafa ya Kifura bw. Shekarata Omary amesema kuwa vijana mpaka kufikia miaka 45 kama wanavyotambuliwa na katiba wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo huku bi upendo Malango ambaye ni afisa tawala wa wilaya ya Kibondo akipongeza kongamano hilo na kwamba vijana wamepata elimu ya kutosha.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amewataka vijana hasa wa kike kutumia vizuri fulsa waliyopewa na raisi Samia ili kujikwamua kimaisha na hatimae kupata maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.