Joy FM

Zaidi ya milioni 400 zajenga daraja, barabara Kigoma

16 September 2024, 10:36

Kiongozi wa mbio za mwenge akikagua daraja la mawe lililojengwa eneo la Mgalaganza Kigoma, Picha na na Tryphone Odace

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava ameutaka uongozi wa halmashauri ya Kigoma kupitia kwa meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA kusimamia na kuweka alama kwenye daraja mawe lilipo katika vijiji vya magalaganza na Mweru ili liweze kutudumu kwa muda mrefu.

Wananchi wanaoishi katika maeneo Mgaraganza na Bweru Katika  Halmashauri ya Wilaya Kigoma  wameipongeza Serikali kwa kuwajengea daraja la mawe ambalo limetajwa kuwa msaada kwa kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

Wakizungumza na redio Fm, mara baada ya mwenge wa uhuru kuzindua daraja hilo la mawe na barabara wamesema kwa sasa usumbufu wa  waliokuwa wakiupata umeisha kwani hapo awali walilazimika kulipia hela ili waweze kubebwa na wakati mwingine mazao yao yakisombwa na maji.

Sauti ya wananchi wa Kijiji cha Mgalaganza wilaya Kigoma

Naye Meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA, wilaya Kigoma Mhandisi Paul Mtapima amesema ujenzi wa daraja hilo la mawe na barabara umegharimu zaidi ya  shilingi milioni mia nne hadi kukamilika kwake.

Sauti ya Meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA, wilaya Kigoma Mhandisi Paul Mtapima

Hata hivyo, Kiongozi wa mbio  za mwenge Kitaifa Godfrey Eliakim Mnzava amemtaka Meneja wilaya kigoma kuhakikisha wanasimamia na kulinda matumizi ya daraja hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu.

Sauti ya Kiongozi wa mbio  za mwenge Kitaifa Godfrey Eliakim Mnzava

Mwenge wa uhuru ukiwa katika halmashauri ya wilaya kigoma  umetembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo  yenye thamani ya shilingi  bilioni 2, ikiwa na lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa  wananchi.

Muonekano wa daraja lililozinduliwa na mwenge wa uhuru katika kijiji cha mgalaganza, Picha na Tryphone Odace