Joy FM

Mbaroni kupanga njama, utapeli na udanganyifu Kigoma

5 September 2024, 16:55

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SACP, Philemon Makungu, picha na Josephine Kiravu

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limesema litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wanaojihusisha na utoaji wa taarifa za uongo iwemo wanaojiteka na kusema wametekwa kwa lengo la kujipatia pesa kwa udanganyifu.

Na Josephine Kiravu – Kigoma

Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia Kocha wa mpira wa miguu Ramadhani Shabani mkazi wa Kichwele kwa tuhuma za kuhusika kupanga njama na kufanya utapeli na udanganyifu kwa kuwalaghai ndugu pamoja na wazazi na kuzua taharuki kwenye jamii.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kigoma SACP Filemon Makungu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kigoma SACP Filemon Makungu

Ameongeza kuwa ni kosa kisheria kufanya udanganyifu kwa lengo la kujipatia fedha huku akimtaja mtuhumiwa mwingine ambaye tayari jalada limefunguliwa aliedai ametekwa na watu wasiojulikana lakini ghafla taarifa zimeonesha yupo jijini Tanga.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kigoma SACP Filemon Makungu

Hata hivyo kamanda makungu amewataka wananchi wenye nia ya kufanya upotoshaji wakidai kutekwa kuacha mara moja huku akieleza kwamba mpaka sasa hakuna tukio la kweli linalohusu utekaji ambalo lipo na kwamba mkoa upo salama wananchi waendelee kushirikiana katika kuibua wahalifu ndani ya jamii.