Joy FM

Baraza la wazee lazitupia lawama sera, sheria zinazotumika kwa sasa

3 September 2024, 15:05

Baraza la wazee katika halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma wameomba kutungwa kwa sheria kutokana na sera ya taifa ya wazee ambayo itawasaidia kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.

Hayo yamejiri katika kikao cha mabaraza ya wazee kutoka kata mbalimbali wilayani Kasulu kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na shirika la endeleza wazee Kigoma EWAKI baadhi ya wazee wamebainisha changamoto mbalimbali wanazokumbanazo katika familia zao.

Sauti za wazee

Afisa ustawi wa jamii kutoka Halmashauri ya mji wa Kasulu Bw.Salumu masaga amesema wazazi wanatakiwa kuwashirikisha watoto wao katika kufanya maamuzi ili kuepuka migogoro ya familia.

Afisa ustawi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Endeleza wazee Kigoma EWAKI Bi, Kotilida kokupima amesema kukosekana kwa vikao vya mara kwa mara kuhusu wazee imekuwa chanzo cha baadhi ya changomoto zao kushindwa kutatuliwa kwa wakati.

Bi, Kotilida kokupima