Joy FM

Rushwa ya ngono inavyowatesa wanawake ziwa Tanganyika

30 August 2024, 13:20

Wanawake wanaochakata mazao ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wamelalamika kushamiri vitendo vya rushwa ya ngono vinavyofanywa na baadhi ya wavuvi kama njia ya kuwapatia mazao ya uvuvi ambapo wameomba kuwezeshwa mikopo ya uhakika, kuepusha athari ikiwemo magonjwa ya zinaa.

Na, Kadislaus Ezekiel,

Ni siku chache tu tangu shughuli za uvuvi kuanza katika Ziwa Tanganyika baada ya kupumzishwa, na sasa wanawake wakiwa katika mkutano wa wadau wa uvuvi na viongozi uliondaliwa na Shirika la Chakula Duniani FAO chini ya mradi wa FISH 4ACP kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine SUA kampasi ya Mizengopinda Katavi, kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika mnyororo uvuvi, wanawake wameomba udhibiti wa vitendo vya rushwa ya ngono ili kufanya uvuvi salama.

Wanawake

Kwa upande wake mmoja wa wavuvi, amekiri uwepo wa vitendo vya rushwa ya ngono akidai ni kutokana na wavuvi wengi kutumia muda mwingi ziwani na kuhama maeneo ya uvuvi.

Hata hivyo mtafiti na mshauri wa masuala ya maendeleo kutoka chuo kikuu cha Sokoine SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi, Profesa Anna Sikira  pamoja na Afisa Uvuvi Wilaya ya Uvinza Haruni Chanda wamewataka wavuvi kuzingatia malezi ya watoto wanaowazalisha na kuwataka kuacha tabia ya kutumia rushwa ya ngono kufanya mauzo ya mazao ya uvuvi.