Joy FM

Zaidi ya wanafunzi 2000 wakatiza masomo Kasulu

30 August 2024, 10:57

Zaidi ya wanafuzi 2000 katika shule za msingi Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wameshindwa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2023 kufuatia changamoto mbalimbali ikiwemo utoro.

Hayo yamebainishwa na Mdhibiti mkuu ubora wa shule halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Sadock Rusekwa wakati akizungumza na wazazi, waalimu na wanafunzi katika shule ya Kalinone english medium pre and primary school ambapo amesema ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha wanasimamia vyema suala la elimu kwa watoto wao ili waweze kutimiza malengo yao.

Mdhibiti mkuu ubora wa shule halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Sadock Rusekwa

Aidha Mwl. Rusekwa amesema serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi, sekondari na vyuo ili kuwasaidia wanafunzi kupata elimu bora na kutimiza ndoto zao.

Mwl, Sadock Rusekwa

Kwa upande wao Wazazi na Walezi kutoka Mjini Kasulu mkoani Kigoma wamesema baadhi ya wazazi wameshindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao baada ya kutoka shuleni hali inayosababisha kushindwa kuhitimu elimu ya msingi.

wazazi