Joy FM

Bajeti ya serikali kutokuwa kikwazo kwenye maendeleo Tanzania

22 August 2024, 15:18

Mashirika yasiyoya kiserikali wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serikali kutoa taarifa kwa wadau wa maendeleo ili kuisaidia serikali kutatua changamoto katika jamii kwa haraka kuliko kusubiri mpangilio wa bajeti ya nchi.

Wameyasema hayo katika kikao cha wadau wa maendeleo kilichofanyika wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Wamesema serikali inapotoa taarifa mapema kupitia vikao vya ndani kwa wadau wa maendeleo pindi changamoto inapotokea inasaidia wadau hao kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kutatua haraka changamoto hiyo.

wadau

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu amesema hakuna tatizo lolote katika kuisaidia serikali kutatua changamoto zilizopo katika jamii, kwani lengo la serikali kusajili mashirika hayo hapa nchini ni kuisaidia serikali kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii ambazo serikali haiwezi kuzigusa kwa mara moja.

wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu

Kanali Mwakisu ameendelea kusema kuwa ndiyo maana hata Mh, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea kuweka mahusiano mazuri kwa wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na serikali katika kuleta chachu ya maendeleo hapa nchini.

wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu