Wanaochoma misitu kuwekwa mbaroni Kasulu
20 August 2024, 12:42
Serikali wilayani kasulu mkaoni kigoma imesema haitaacha kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wotw wanaojihusisha na uharibifu wa mazingira kwa kuchoma moto.
Na Michael Mpunije – kASULU
Wadau wa maendeleo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameshauriwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha jamii utunzaji wa mazingira ili kuepuka kuchoma misitu moto na kuona umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu katika kikao cha jukwa la mwaka kwa mashirika ya siyo ya kiserikali NGOs ndani ya ukumbi wa mikutano wa mkuu wa wilaya ya hiyo.
Amesema lengo la kuwashirikisha wadau hao wa maendeleo ni kufuatia baadhi ya wananchi kuchoma misitu moto kutokana na fikra hasi hali inayopelekea uharibifu wa mazingira ndani ya wilayani hiyo.
Aidha Kanali Mwakisu amesema serikali tayari imeandaa mpango wa kuwakamata wale wanaochoma misitu moto.
Kwa upande wake Mkuu wa diviseni ya kilimo mifugo na uvuvi halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mikidadi Mbaruku amezungumzia madhara yanayotokea baada ya kuchoma misitu moto ikiwemo uharibifu wa udongo.
Nao baadhi ya wadau wa maendeleo wilayani Kasulu wamesema wanatambua umuhimu wa kutunza mazingira huku wakionyesha utayari wao wa kushirikiana na serikali katika suala hilo.