Madereva kuvaa mavazi kukinga upepo kuepuka kifua kikuu
14 August 2024, 14:47
Shughuli ya udereva wa pikipiki licha ya kuwa shemu ya chanzo cha mapato kwa vijana walio wengi lakini kuktotii sheria za kuvaa jaketi za kukinga upepo huenda ukawa changamoto kwao kutokana na maambukizi ya kifua kikuu kinachosababishwa na upepo wakati akiendesha pikipiki.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Waendesha pikipiki wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuvaa mavazi yakuwakinga na upepo mkali ili Kuepuka kupata ugonjwa wa kifua kikuu.
Akizungumza na waendesha pikipiki wilayani Kasulu kwa niaba ya DTO wa wilaya hiyo SGT Sabato Rajabu amesema ipo hatari kubwa kwa baadhi ya waendesha pikipiki ambao wanashindwa kuvaa vikinga upepo wakati wa shughuli za usafirishaji.
SGT Sabato amesema serikali inahakikisha waendesha pikipiki wanakuwa salama ili kuepuka kupoteza nguvu kazi ya Taifa kutokana na magonjwa ya kifua kikuu ambayo husababishwa na upepo mkali kutokana na kushindwa kuvaa mavazi ya kukinga upepo kwa baadhi ya waendesha pikipiki.
Aidha SGT Sabato amewataka waendesha pikipiki kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani huku akiwakumbusha kuvaa miwani ili kukabiliana na wadudu wanaoweza kusababisha ajali.
Baadhi ya waendesha pikipiki wilayani Kasulu wamesema usalama unatakiwa kuanzia kwa mtu binafsi kuhakisha anavaa jaketi zito ambalo litamsaidia kujikinga na baridi pamoja na kuendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na maafisa wa usalama barabarani.