Barabara ya Buhigwe-Kasulu kunufaisha wananchi kiuchumi
12 August 2024, 13:56
Wananchi wa kata ya Heru Juu katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wameipongeza serikali kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya lami unaoendelea kutoka wilayani Buhigwe kuelekea wailayani Kasulu ambapo ukikamilika utawasaidia katika shughuli zao za kiuchumi.
Pongezi hizo wamezitoa wakati wakizungumza na radio joy fm katika kata hiyo ambapo wamesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo itasaidia katika shughuli za uzalishajimali.
Aidha wameiomba serikali kuongeza kasi ya ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati uliokusudiwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu ambaye pia ni Diwani wa kata ya Heru Juu Noel Hanura Buliho licha ya kuipongeza serikali kwa hatua hiyo ya ujenzi wa mradi wa barabara unaoendelea, amewaomba wananchi kuwa makini wakati wa kuvuka barabara hiyo ili kuepuka ajali zisizokuwa na ulazima.
Sambamba na hilo Mh. Hanura amesema ujenzi huo wa barabara ya lami utakapokamilika unakwenda kuufungua mkoa wa Kigoma kibiashara