Joy FM

Dkt. Nchimbi, hatutaki mchakato, wananchi wanahitaji kituo cha afya

6 August 2024, 10:52

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma Mh Asa Makanika ameiomba serikali ya awamu ya sita  kusaidia wananchi wa kata ya Mwandiga  Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuwajengea kituo cha afya ili kuondoa usumbufu wanaoupata wakati wakihitaji matibabu.

Kauli hiyo ameitoa mbele ya katibu mkuu wa chama cha CCM Ndgu:Emmanuel Nchimbi  wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali mkoani hapa, kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali  wanazozipata wananchi

Naye katibu mkuu wa CCM taifa Ndgu: Emmanuel Nchimbi amewatoa hofu wananchi wa kata ya mwandiga kuwa mchakato wa ujenzi utaanza kufanyika mara moja na kumpongeza mbunge wao kwa kufanya kazi kwa bidii kwaajili ya jamii na kusisitiza wizara  ya TAMISEMI kufanyia kazi jambo hilo ili kuondoa adha kwa wakazi hao.

Aidha, katibu mkuu ameelekeza wizara ya nishati kuongeza kasi kwaajili ya wananchi wa kigoma vijijini kwa kuwasogezea huduma ya umeme.