Joy FM

Bilioni 58.7 zaboresha sekta ya elimu Kigoma

6 August 2024, 10:08

Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba ya katibu mkuu wa CCM Taifa. Picha na Hamis Nterekwa

Na, Joha Sultan

Naibu Waziri Ofisi ya Raisi wizara ya Tamisemi Mhe.Zainabu Katimba amewataka wazazi wote mkoani kigoma kuwapeleka watoto shule na kukomesha utoro.

Ameeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanywa na chama cha mapinduzi katika viwanja vya community center mkoani kigoma ambapo amesisitiza wazazi kukomesha utoro kwa watoto ili kupata elimu bora.

Aidha  Mhe, Katimba amesema katika kipindi cha miaka mitatu jumla ya shilingi Bil 58.7 kuboresha sekta ya elimu na kuboresha miundombinu ya elimu  kwa kujenga shule mpya, ukarabati wa vyumba vya  madarasa  na kuboresha miundo mbinu ya vyoo.

Hata hivyo mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni Katibu mkuu chama cha mapinduzi CCM Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi ameitaka serikali kuendelea kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na kudumisha amani bila kujali udini na ukabira wala uchama.