Serikali yapongezwa kuimarisha ulinzi usafiri wa usiku
2 August 2024, 11:18
Uamzi wa serikali kuruhusu magari kuanza safari za usiku kwenda maeneo mbalimbali ya nchi hofu ziliibuka kwa baadhi ya wananchi wakihofia usalama wakati wa safari kitu ambacho serikali chini wizara ya mambo ya ndani iliwatoa hofu wananchi na kuwa wataimarisha ulinzi na sasa safari zinaendelea kukiwa hakuna hofu ya kusafiri usiku.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa na askofu wa DWT kwa kuimarisha ulinzi na usalama nchini hali inayopelekea baadhi ya mabasi kusafiri usiku kutokea mkoani Kigoma.
Pongezi hizo zimetolewa na Mhashamu askofu Emmanuel Bwatta wa kanisa la anglikana Tanzania dayosisi ya western tanganyika yenye makao makuu yake Kasulu Mjini Mkoani Kigoma.
Amesema kuimalishwa kwa ulinzi na usalama nchini imesaidia kuongezeka safari za mabasi ya kuelekea mikoani kutokea mkoani kigoma hali ambayo imeondoa changamoto ya kusafiri alfajiri.
Aidha askofu Bwatta ameishukuru serikali kwa namna inavyopeleka maendeleo kwa jamii ikiwemo ujenzi wa barabara za lami na ujenzi wa madarasa pamoja na ujenzi wa zahanati na vituo vya afya.
Kwa upande wao baadhi ya wasafiri na wakazi wa wilayani Kasulu akiwemo Uzia Gabriel, Asifiwe Zaledi, Julius Lameck na Mchungaji Ngeze Mzimya wamesema serikali imefanya jambo jema lakini inatakiwa kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wakati wote wa safi hizo.