KUWASA yalalamikiwa maji kuwanufaisha matajiri tu Kigoma
1 August 2024, 11:24
Wananchi Katika Kijiji cha Matyazo Kata ya Kalinzi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma, Wamelalamika kukatiwa Maji kutoka katika Mradi wa Maji Kijiji humo, na kusababisha kaya nyingi kulazimika kutumia maji yasiyosalama kiafya, sambamba na kuomba Uongozi wa RUWASA kuchukua hatua kuchunguza sababu za mradi wa maji kushidwa kutoa huduma katika baadhi ya magati.
Katika Mkutano wa hadhara, uliohusisha Viongozi ngazi ya Wilaya Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Assa Makanika, Wananchi wa MATYAZO, wameeleza Kukosa huduma ya maji safi na salama, kwa madai kuwa magati mengi yaliyokuwa yanatoa huduma kupitia mradi wa maji Kijiji humo hayatoi huduma kwa sasa, na kuacha maswali mengi kwa jamii.
Suala hilo, likamfanya Mbunge Assa Makanika kumtaka Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Vijiji RUWASA Wilaya ya Kigoma Mhandisi Yesaya Elya ambapo amekili mradi kushidwa kutoa huduma kwa wananchi kulingana na ongezeko la watu, na unaandaliwa utalatibu wa mradi mpya utakao kidhi mahitaji.
Kisha Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Assa Makanika, ametoa maelekezo ya kuchimba kisima kusaidia upatikanaji wa maji wakati, mchakato wa ujenzi wa mradi mkubwa ukiendeela na kurahisisha upatikanaji wa maji kwa wananchi.