Wananchi kunufaika na kilimo cha umwagiliaji mto Luiche Kigoma
22 July 2024, 15:27
Na, Emmanuel Michael
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewataka wananchi katika kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma kutouza ardhi yao ya kilimo katika Bonde la Mto Luiche ambalo limekuwa kitovu cha uchumi wao baada ya serikali kukabidhi eneo la mradi wa umwagiliaji kwa mkandarasi ili kuanza ujenzi wa skimu ya kilimo cha umwagiiliaji
Sera ya taifa siku zote imekuwa ni kukifanya kilimo kuwa sehemu ya mtanzania kujikwamua kiuchumi na ndiyo maana inaelezwa kuwa kilimo ni uti wa mgongo
Bonde la Mto Luiche limejumuisha wakulima mbalimbali wakiwemo wa mazao ya mpunga, mahindi, mbogamboga na matunda.
Hili ni bonde linalotajwa kuwahudumia wakulima 9312 ambapo mradi huu wa umwagiliaji Luiche utajengwa na unajumuisha maeneo mawili ambayo ni skimu ya umwagiliaji na ujenzi wa bwawa la lita za ujazo laki 7 na kumi.
Na hapa wanufaika wa moja kwa moja ambao ni wakulima wanaeleza namna ambavyo mradi huo unakwenda kuwanufaisha.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mradio wa umwagiliaji Meneja Mradi wa Luiche Katuta Mustang amesema mradi huo unatarajia kutumia shilingi bilioni 60 na utatumia siku 720 sawa miaka miwili ili kukamilka ambapo ujenzi umeanza Julai 21 mwaka huu huku Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa akisistiza juu ya utunzwaji wa mazingira.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema hatua hiyo kubwa kwa wakulima inakwenda kuongeza chachu ya maendeleo kupitia kilimo.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewataka wananchi kutouza maneo yao kwa kurubuniwa kwani maeneo hayo thamani yake itawainua kiuchumi.
Eneo hilo hekta 2800 zitalimwa mpunga, mahindi hekta 150.