Mwenyekiti UWT aingilia kati ukosefu wa maji Kigoma
19 July 2024, 13:40
Mamlaka ya maji safi na usafii wa mazingira manispaa ya kigoma ujiji, imetakiwa kuhakikisha inajenga kituo kipya cha kusambaza maji kwa wananchi wa kata ya mji mdogo wa mwandiga katika halmashauri ya wilaya kigoma ili kuwasaidia wananchi kuepukana na matumizi ya maji yasiyokuwa safi na salama.
Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma
Mwenyekiti wa Umoja Wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi Ccm Taifa, Mary Chatanda ameagiza Watendaji wa waserikali wa idara ya maji kusaidia utatuzi wa changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika kata ya Mwandiga Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, na kusisitiza taratibu za kuwajengea mradi wa maji zianze mara moja.
Bi. Chatanda amesem hayo wakati wa mkutano na wananchi wa kata ya Mwandiga ambao wamelalamikia ukosefu wa maji safi na salama kwa kukosa mradi wa kusambaza maji toshelevu kata hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA Poas Kilangi, amesema kuwa tayari ameomba Serikali kiasi cha Bilioni Mbili ambazo zitatumika kujenga mradi wa maji toshelevu ambao utaweza kufikisha maji kwa wananchi huku Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amesema, atahakikidha anafuatilia hatua zote, ili wananchi wa Mwandiga waweze kupata maji bila usumbufu.
Aidha Mkuu wa wilaya kigoma amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma karibu za kijamii.