NGO’s zilivyoinua uchumi Kasulu
19 July 2024, 11:36
Serikali imesema uwepo wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ndani ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma imekuwa na mchango mkubwa katika kuchochea suala la maendeleo.
Hayo yameelezwa na Bi. Theresia Mtewele katibu tawala wa wilaya ya Kasulu wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserikali katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji Kasulu.
Amesema uwepo wa mashirika hayo katika wilaya ya Kasulu imekuwa chachu ya maeneleo katika ukuaji wa uchumi hali inasasaidia kupunguza changamoto ndani ya jamii.
Bi. Mtewele amewasisitiza wanapoendelea na shughuli zao wazingatia mila na desturi za kitanzania ili kuepuka suala la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa mashirika hayo ya siyo ya kiserikali wamesema nchi ina mifumo mizuri lakini utekelezaji wake ndio tatizo.