Joy FM

Nabii awaonya waumini kutegemea miujiza

18 July 2024, 11:50

Waumini wa dini ya kikristo mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata mafanikio ambayo yatawasaidia katika maisha yao kuliko kutegemea miujiza.

Hayo yameelezwa na Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya western Tanganyika Mhasham Emmanuel Bwatta wakati akizungumza na waumini wa kanisa hilo Mjini Kasulu.

Maandiko yanasema “Asiye fanya kazi na asile” ndivyo Askofu Bwatta amewahimiza wakristo mkoani Kigoma kufanya kazi kwa bidii na kuacha kutegemea miujiza.

Askofu Bwatta amesema watu wana nguvu na afya njema lakini bado baadhi yao wamekuwa wakitegemea kupokea miujiza jambo linalowachelewesha kufikia mafanikio yao.

Askofu Emmauel Bwata

Kwa upande wake Mtumishi wa Mungu Nabii Joel Philipo kutoka huduma ya International Evagelism Kisima cha makimbilio Mkoani Kigoma amesema hakuna kupokea pasipo kufanya kazi na unapomwambia mtu pokea lazima umfundishe na mfumo wa ufanyaji wa kazi.

Joel Philipo

Kwa upande wao baaadhi ya waumini wa dini ya kikristo wilayani Kasulu wameunga mkono kauli ya askofu Bwatta na kusema jamii inatakiwa kuamka kutoka usingizini nakutambua umuhimu wa kufanya kazi.

waumini