Wapanda juu ya miti kutafuta mawasiliano Geita
18 July 2024, 11:40
Serikali imesema itaendelea kujenga minara nchini nzima ili kuhakikisha mawasiliano yanapatikana kwa wananchi waliokuwa hawapati mawasiliano ili kuchochea maendeleo.
Na Samwel Masunzu
Wananchi wa kata ya Nyakagomba wilayani Geita mkoani Geita wamesema walikuwa wanalazimika kupanda kwenye vichuguu na milima kutafta urahisi wa mtandao kutokana na changamoto iliyokuwepo ya kutokuwa na manara wa simu kwenye eneo lao.
Wananchi hao wameeleza hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Mawasliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ya kukagua minara ya mawasliano inayojengwa kwa fedha za ruzuku kutoka serkalini.
Wamesema kwa sasa baada ya mnara kujengwa huduma za mawasliano zimekuwa rafiki.
Naye waziri Nape Nnauye amesema mnara huo ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 130, hautakuwa na maana kwa wananchi kama hawatautumia vyema.