Wananchi walia na TANESCO kutopewa umeme
18 July 2024, 09:07
Mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini Assa Makanika amelitaka shirika la umeme mkoani kigoma TANESCO kuhakikisha wanapeleka huduma ya umeme kwa wananchi wa vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo hali inarudisha nyuma shughuli za maendeleo.
Na Kadislaus – Kigoma Dc
Wananchi katika vijiji vya kata ya Mkongoro Halmashauri Ya Wilaya Ya Kigoma Mkoani Kigoma, wamewatuhumu viongozi wa TANESCO wilayani humo, kuwachukulia fedha zao Ili kupatiwa UMEME wa REA, huku wakiwatelekeza bila huduma kutolewa, na wengine kuingia hasara ya kununua vifaa vya umeme wakiwa na uhakika wa kupata nishati hiyo.
Wakizungumza katika mkutano wa viongozi, wananchi na mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini mheshimiwa assa makanika, ambapo wananchi wa kata ya mkongoro wamelalamikia baadhi ya viongozi wa tanesco kuwatoza fedha wananchi, ili kuletewa nishati ya umeme bila mfanikio.
Jambo hilo linamfanya mbunge assa makanika, kumtaka mhandisi wa umeme wilaya ya kigoma josephu kanje na kutolea ufafanuzi.
Aidha mbunge Assa Makanika, akatoa maelekezo ya jumla kuhakikisha tanesco wanachukua hatua za kuwapeleka umeme wananchi ambao hajanifaika na huduma hiyo.