Waumini wa kikristo kugombea nafasi za uongozi Kigoma
12 July 2024, 13:18
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika mhasham Emmanuel Charles Bwatta amewashauri waumini wa dini ya Kikristo mkoani Kigoma kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu.
Askofu Bwatta amesema hayo wakati akizungumza katika ibada ya uzinduzi wa kanda mpya ya Kasulu mjini ya Kanisa hilo iliyofanyika hapo jana kanisa la Kristo mfalme anglikana Murusi.
Amesema waumini wa kikristo wanapaswa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo za serikli za mitaa ili kugombea nafasi za uongozi.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Lake Tanganyika Theorojiko College LTC cha Kanisa hilo Mchungaji Alberto Koruza amesema hamasa hiyo ni kutokana na kuona miongoni mwa waumini wamekuwa wakishindwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi.
Nao baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo wamesema ni vizuri kuwapata viongozi wenye hofu ya Mungu ili waweze kusimamia maendeleo kwa wananchi yanatolewa na serikali.