Joy FM

Hii hapa ahadi ya Bashungwa kwa makamu wa rais Dr Mpango

11 July 2024, 12:54

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Philip Isdor Mpango amemtaka waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kuhakikisha upanuzi wa uwanja wa ndege unakamilika haraka ifikapo 2025.

Na Josephine Kiravu
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifanya ukaguzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege Kigoma mradi ambao awali ulipaswa kukamilika mwezi march 2025.
Makamu wa Rais amesema ili kuufungua Mkoa wa Kigoma kiuchumi ni lazima miundombinu ya barabara pamoja na uwanja wa ndege viwe rafiki.

Awali akieleza kuhusu hatua za utekelezaji wa mradi huo Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema awali mradi huu ulipaswa kuwa chini ya TIA na ulipaswa kukamilika march 25 lakini baada ya kutokea changamoto ambapo mkataba ulipaswa kusainiwa 2018 lakini mwaka 2023 mradi ulipelekwa TANROADS na ndio wanatekeleza mradi Hadi sasa.

Waziri wa ujenzi :Innocent Bashungwa

Ameongeza kuwa kwa Kasi ambayo mkandarasi anaenda nayo mradi huu utakamilika mwezi December 2025.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ametembelea eneo inapojengwa hospital ya Kanda ya magharibi pamoja na chuo kikuu Cha Muhimbili ambapo amejionea namna ujenzi utakavyokuwa huku akimtaka mkuu wa Mkoa kuona namna ya kuboresha eneo Hilo kwa kupanda miti.
Hata hivyo Makamu wa Rais akiwa njiani kuelekea Kijiji Cha Kasumo amesikiliza changamoto za wananchi wa kata za Kalinzi na Mnanila ambapo ameahidi kuzifanyia kazi.

Makamu wa Rais amehitimisha siku ya pili ya ziara yake hii Leo na anatarajia kuendelea na ziara hii Mkoani Kigoma July 13 mwaka huu.