Joy FM

Askofu wa Anglikana Tanzania awanyoshea kidole wazazi

9 July 2024, 13:17

Wazazi na Walezi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma imeaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kuwa viongozi bora wa baadae.

Mhashamu baba askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya western Tanganyika mkoani Kigoma Emmanuel Bwatta ametoa rai hiyo katika mahafari ya wanafunzi wa ukwata katika shule ya Msingi Gahima iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Amesema unapomlea mtoto katika maadili mema itamsaidia kufanya vizuri katika masomo yake na kuishi vyema na jamii inayo umzunguka.

Askofu Emmanuel Bwata

Aidha Askofu Bwatta amewasisitiza wanafunzi wanaoelekea kuhitimu darasa la saba kusoma kwa bidii pamoja na kumtegemea Mungu katika maisha yao ya kila siku ili kuwa mfano bora katika jamii.

Askofu Emmanuel Bwata

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Gahima George Paul amewaomba wazazi kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwapa malezi bora ambayo yatakuwa darasa kwa jamii inayowazunguka.

Mwalimu Mkuu: George Paul

Naye Dorcas Wilfred ambaye ni mzazi aliyewawakilisha wazazi wengine waliohudhuria katika mahafari hayo ya ukwata amesema wamepokea ushauri huo kutoka kwa Baba Askofu kuhusu kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wafanikiwe katika maisha yao.

Mzazi