Joy FM

Tuzo kwa walimu kuchochea ufaulu kwa wanafunzi Kigoma

9 July 2024, 10:58

Waalimu wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuongeza bidii na maarifa katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye katika hafla ya utoaji motisha kwa baadhi ya  waalimu wa shule za msingi na sekondari kutoka kata ya Murusi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Bogwe kwa lengo la kuwahamasisha kufanya kazi hiyo kwa wito ili kutimiza ndoto za wanafunzi

Amesema kiongozi bora ni yule anayefanya kazi kwa kufuata misingi, sheria na taratibu bila kuathiri maslahi na haki za walio chini yake.

Mkurugenzi mji Kasulu :Mwl Vumilia Simbeye

Aidha Mwl. Simbeye amewapongeza waalimu wanaotimiza majukumu yao kwa wakati katika kuinua sekta ya elimu ndani halmashauri hiyo.

Mkurugenzi mji Kasulu :Mwl Vumilia Simbeye

Kwa upande wake afisa elimu wa kata ya Murusi Gervas Mgeze aliyeandaa motisha hiyo kwa waalimu hao licha ya kuwataka waalimu hao kuwa mabalozi kwa jambo hilo amesema motisha hiyo itasaidia kuboresha sekta ya elimu ndani ya kata ya Murusi na wilaya ya Kasulu kwa ujumla.

Afisa elimu kata ya murusi :Gervas Mgeze

Nao baadhi ya waalimu walioshiriki katika hafla hiyo akiwemo mwalimu Mahona Byura kutoka shule ya sekondari Hwazi, Rose Kibindi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kasulu na Peter Mwakitaru kutoka shule ya msingi Kasulu wamesema mahusiano mazuri ya kikazi yanasaidia utendaji kazi bora katika kuleta maendeleo.

Waalimu

Katika hafla hiyo waalimu kumi na tisa wamepewa tuzo kwa namna wanavyotekeleza wajibu wao ili kusaidia sekta ya elimu ndani ya kata ya Murusi.