Joy FM

Dkt. Mpango akabidhi magari matano kwa MADC Kigoma

9 July 2024, 11:34

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania akikata utepe katika hafla ya kukabidhi magari kwa wakuu wa wilaya tano za kigoma, Picha na OMR

Wakuu wa wilaya mkoani kigoma wametakiwa kuwatembelea na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ili kuhakikisha wananchi wanapat huduma kwa wakati.

Na Josephine Kiravu – Kigoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Dr Philip Isdor Mpango amekabidhi magari matano kwa wakuu wa wilaya za Uvinza, Kasulu, Kibondo, Kakonko na Kigoma kwa ajili ya kurahisisha kuwafikia wananchi na kusikiliza pamoja na kutatua kero zao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo Makamu wa Rais amesema bado baadhi ya viongozi hawatekelezi majukumu Yao ipasavyo huku akiwataka kuhakikisha wanawafikia wananchi na kutatua changamoto zao.

Sauti ya makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango

Insert…..Dina

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dina Mathamani amesema jukumu lake ni kuwafikia wananchi na kwamba kupitia gari ambalo amekabidhiwa litaongeza chachu na kurahisisha kuwafikia wananchi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Uvinza Dina Mathamani

Mh Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo Mkoani Kigoma ambapo atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya.

Muonekano wa magari matano yaliyokabidhiwa kwa wakuu wa wilaya, Picha na ONR