Joy FM

Ukosefu wa maji wasababisha ndoa kuvunjika

4 July 2024, 13:05

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira KUWASA akiwa na wananchi wa kata ya kalalngabo, Picha na Emmanuel Matinde

Wanawake wa kijiji cha kalalangabo wamesema kukoekana kwa huduma ya maji umesababisha wanaume zao kuwakimbia kwa kile wanadai kuwa wanatoa harufu na kuamua kwenda nje ya ndoa.

Na Emmanuel Matinde – Kigoma

Wakazi wa Kijiji cha Kalalangabo Kata ya Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, hivi karibuni wanatarajia kuondokana na shida ya ukosefu wa maji safi na salama iliyowakabili kwa muda mrefu tangu kijiji hicho kuanzishwa baada ya uhuru.

Kilio cha wananchi wa kijiji cha Kalalangabo kuhusu maji kitakwisha mara baada ya kukamilika kwa uboreshaji wa chanzo kidogo cha maji katika eneo la Kibirizi ambapo unafanyika uwekaji wa pampu ya kusukuma maji kutoka chanzo kikuu cha maji cha Amani Beach na kuingia katika tenki la lita laki moja na nusu ambalo litasambaza maji kijijini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA, Poas Kilangi, Picha na Emmanuel Matinde

Kulingana na taarifa ya ujenzi wa chanzo hicho kwa sasa kazi hiyo imefikia asilimia 80% lakini tayari wananchi wa kijiji hicho wameonyesha imani kubwa kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA, hasa baada ya wao wenyewe kutembelea eneo la chanzo na kujionea kazi inayoendelea kufanyika.

Sauti ya wananchi wa kijiji cha Kalalangabo

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA, Poas Kilangi, amesema baada ya mamlaka kupokea kilio cha wananchi hao ofisi yake ilitenga fedha Shilingi Milioni 160 za mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji huduma ya maji kwa wakazi wa kijiji cha Kalalangabo.

Sauti ya mkurugenzi wa maji KUWASA