Joy FM

Wananchi Kasulu waomba doria kudhibiti uhalifu

2 July 2024, 10:57

Baadhi ya viongozi wa kata ya Mwilamvya wakiwa katika mkutano wa kujadili masuala ya maendeleo ya kata, Picha na Michael Mpunije

Jeshi la polisi wilayani Kasulu limesema litaendelea kufanya doria muda wote ili kuweza kuwatia hatiani watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kwenye makazi ya watu.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Wananchi wa kata ya Mwilamvya halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wameliomba jeshi la polisi wilayani Kasulu kuendelea kufanya doria na misako mbalimbali ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika baadhi ya maeneo wilayani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwilamvya mmoja wa wananchi wa kata hiyo Bw. Alinatius Josephu amesema vitendo vya wizi na uporaji vinazidi kuongezeka hali inayohatarisha usalama wa wananchi.

Bw. Joseph ameliomba jeshi la polisi kuongeza mtandao wa kusaka wa halifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa simu pamoja na kuwapora mikoba wanawake.

Sauti ya mwananchi wa kata ya Mwilamvya

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Kasulu Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kasulu Sperius Felix Rweyemamu amesema wanaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote kwa kufanya misako na doria usiku na mchana ili kuhakikisha wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakatwa na kufikishwa mahakamani.

Sauti ya Mkuu wa polisi wilaya ya Kasulu Msaidizi wa Mkuu wa upelelezi wilaya ya Kasulu Sperius Felix Ruemamu

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Mwilamvya Bw. Ramadhani Shabani amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia.

Sauti ya afisa mtendaji wa kata ya Mwilamvya bw.Ramadhani Shabani