Wananchi Kasulu walia mabomba kutoa maji machafu
2 July 2024, 10:42
Wananchi wa kata ya Kumunyika wamelalamikia serikali kupitia mamlaka ya maji Kasulu kuruhusu mabomba ya ya maji kuwa na tope hali inayoweza kusababisha magonjwa ikiwemo kuhara.
N a Emmanuel Kamangu – Kasulu
Diwani wa kata ya Kumunyika Bw. Selaman Kwirusha amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kasulu KUWASA kushughulikia kwa wakati kero ya baadhi ya wananchi wa kata ya Kumunyika kukabiliwa na utumiaji wa maji machafu yanayotoka katika mabomba.
Katika mkutano huo ambao umeandaliwa na Diwani wa kata ya Kumunyika Bw. Kwirusha wananchi wa kata hiyo wakaibua kero mbalimbali ikiwemo kukabiliwa na utumiaji wa maji machafu yanayotoka katika mabomba ambapo wamedai wamekuwa wakiugua minyoo na magonjwa ya kuhara na kufuatia changamoto hiyo kaimu mkurugenzi wa KUWASA Bw. Guttu Bundara akayatolea ufafanuzi.
Aidha Diwani wa kata ya Kumunyika Bw, Seleman Kwirusha ameeleza mafanikio ambayo wamefanikiwa katika kata hiyo yenye mitaa mitano ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari na msingi sambamba na uwepo wa barabra ya kuwaunganisha wananchi wa kata ya Kumunyika pamoja na wananchi wa kata ya Mhunga.
Hata hivyo wanyeviti wa mitaa katika kata ya Kumunyika wametumia fursa ya mkutano huo wa hadhara kuwaaga wananchi wao huku wakiwaomba waendelee kuwaunga mkono katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ili waendelee kuwawakilisha.