Joy FM

Shule zatakiwa kulima ili kupata chakula cha wanafunzi

27 June 2024, 09:25

Baadhi ya wakulima wakiwa katika zoezi kupakia mahindi yaliyovunwa shambani, Picha na Mtandao

Katika kukabiliana na tatizo la chakula kwa wanafunzi shuleni wilayanikasulu, shule za msingi na sekondari wametakiwa kuanzisha mashamba ili waweze kulima na kupata chakula cha kutosha.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Shule za msingi na Sekondari katika halmashauri ya wilaya ya kasulu Mkoani Kigoma zimetakiwa kuanzisha mashamba ya shule kwa kupanda mazao mbalimbali ya chakula ili kupunguza mzigo kwa wazazi kuchangia chakula shuleni.

Wito huo umetolewa na afisa Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu bw.Kingolo sayi wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,wazazi pamoja na waalimu wakuu wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri hiyo.

Bw.Kingolo amesema baadhi ya shule tayari zimeshaanzisha mashamba ili kusaidia upatikanaji wa chakula na kwamba suala hilo limesaidia kwa baadhi ya wazazi ambao hawana uwezo wa kuchangia chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wao  kutokana na hali duni ya maisha.

Sauti ya afisa Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu bw.Kingolo sayi

Aidha bw. Kingolo ameongeza kwa kuwataka wazazi na walezi kuzingatia lishe bora kwa watoto ili kukabiliana na utapiamlo.

Sauti ya afisa Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu bw.Kingolo sayi

Hivi Karibuni akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya kasulu Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Bw.Hassan Rugwa alibainisha kuwa changamoto ya utoro kwa wanafunzi imekuwa kubwa huku wengine wakiacha shule kutokana na sababu mbalimbali miongoni ikitajwa kuwa ni ukosefu wa huduma ya chakula shuleni ambapo amewataka madiwani kuhamasisha wazazi kuendelea kuchangia chakula mashuleni.

Sauti ya Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Bw.Hassan Rugwa
Ni Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Bw.Hassan Rugwa