Walimu waaswa kutofanya kazi kwa mazoea
27 June 2024, 09:00
Halmashauri ya wilaya Kibondo imetakiwa kutatua mahitaji ya walimu na kuacha kutumia lugha zisizo rafiki kwa walimu wanapopeleka changamoto zao ili zitatuliwe.
Na James Jovin – Kibondo
Katika kurekebisha upatikanaji wa elimu bora hapa nchini walimu wilayani Kibondo wameaswa kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea ili kufikia malengo ya serikali na kuwapatia Watoto ujuzi utakaowasaidia katika Maisha
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi upande wa Elimu Charles Msonde alipokuwa akizungumza na Walimu wa shule za Msingi na sekondari wilayani Kibondo Mkoani Kigoma ambapo amesema Mkoa huo uko kiwango cha chini kielimu kutokana na ufundishaji usiozingatia vigezo.
Amesema kila mwalimu anatakiwa kujipima utendaji wake wa kazi kwa kuwasaidia wanafunzi na kuwataka kuacha mazoea kazini.
Baadhi ya walimu walioshiriki kikao hicho wamekili uwepo wa utendaji usioridhisha na baada ya kupata maelekezo wameahidi kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Pamoja na mambo mengine Msonde ameitaka halmashauri ya kibondo kutatua mahitaji ya walimu na kuacha kutumia lugha zisizo rafiki walimu wanapopeleka changamoto zao ilizitatuliwe